MAN UNITED KUMPIGA BEI DANNY WELBECK …huenda akatimkia Tottenham au Arsenal


MAN UNITED KUMPIGA BEI DANNY WELBECK …huenda akatimkia Tottenham au Arsenal

Down the pecking order: Danny Welbeck could leave                    United in search of regular first-team football

MSHAMBULIAJI wa Manchester United Danny Welbeck huenda akapigwa bei iwapo dili la usajili wa Angel Di Maria kwenda Old Trafford litakamilika.

United inakaribia kumnasa Di Maria kwa pauni milioni 50 kutoka Real Madrid. PSG ni kama imejitoa kwenye dili hilo huku Real Madrid ikiwa haina mpango wa kumuuza winga huyo Barcelona.

Kama Di Maria atatua Old Trafford, basi nafasi ya Welbeck kwenye kikosi cha kwanza cha United itakuwa imefifia.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England anawaniwa na Tottenham kwa pauni milioni 15 – lakini mshahara wake wa pauni 80,000 kwa wiki unaweza kuwa tatizo kwa mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy.

Arsenal pia wanatajwa kuwania saini ya mshambuliaji huyo wa United.



Comments