Jumla ya makundi kumi yamefanikiwa kuingia katika mchuano wa nusu fainali ya shindano la Dance 100% shindano hilo linaloandaliwa na kituo cha (EATV) chini ya udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania,yanaendelea kupamba moto ambapo hapo juzi hatua ya robo fainali ilifanyika katika uwanja wa Don Bosco Mbuyuni Namanga jijini Dar es Salaam na makundi 10 yalifanikiwa kuchukua tiketi ya kuingia nusu fainali.
Mratibu wa shindano hilo Happy Shame aliyataja makundi yaliyofanikiwa kuingia nusu fainali kuwa ni Wazawa Crew,Best Boys Crew,G.O.P,The WT,Tatanisha Dancers, Quality Boys, Wakali sisi, Mazabe Powder,The Winners Crew, Dar Crew, Mratibu wa mashindano hayo,Happy Shame,alisema kuwa amefuhishwa na juhudi zinazofanywa na washiriki katika shindano hilo na anawapa pongezi sana majaji kwa kuwa makini na kuweza kupata makundi 10 rasmi yaliyoingia moja kwa moja ngazi ya nusu fainali.
"Huu ni mwaka wa tatu East Africa Televisheni tunaandaa mashindano haya kwa udhamini wa Vodacom Tanzania na Mwaka huu tumeungwa mkono na Grand Malt kama kinywaji rasmi cha Dance 100%. Kwa kweli nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitaweza kutoa shukururani zangu kwa wadhamini kwani wasingekuwa wao tusingekuwa hapa tulipo"Alisema Happy.
Happy, aliongeza kwamba kundi litakaloibuka na ushindi katika mashindano haya ambayo pia yamekuwa yakionyeshwa na kituo cha televisheni cha EATV kila jumatano saa moja kamili usiku,litajishindia kitita cha shilingi milioni 5.
Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano haya,Matina Nkurlu alisema kuwa Vodacom inatoa udhamini kwa kutambua kuwa muziki na michezo ni maeneo ambayo yanaweza kutoa ajira sahihi kwa vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha.
Alisema kuwa kwa niaba ya Vodacom Tanzania,anayapongeza sana makundi hayo 10 yaliyoingia nusu fainali na kwa kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote ikiwemo makampuni,taasisi za umma na za binafsi basi wanajisikia fahari sana kwa vijana hao kuingia nusu fainali ndio maana siku zote Vodacom imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na tatizo la ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo , burudani.
"Vodacom tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa hivyo tunadhamini mashindano haya tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia katika sanaa"Anasema Nkurlu.
Alisema jinsi siku zinavyoenda ndiyo jinsi anavyowaona vijana wanaoshiriki katika shindano hilo wamekuwa makini kwa kile wanachokifanya kwani wametambua kuwa michezo ni ajira na wanaitumia fursa hii waliyoipata ipasavyo ili waweze kujikomboa kiuchumi "Suala la ajira kwa vijana sio lazima kufanya kazi viwandani au maofisini tu bali kuna njia nyingi za kujiajiri na kujipatia kipato mojawapo ikiwa ni kupitia michezo,muziki na sanaa nyingine na Vodacom siku zote tupo mstari wa mbele kuinua vipaji vya vijana na kuweza kujikwamua kiuchumi"Alisisitiza Nkurlu.
Kikundi cha Quality Boys cha Kinondoni jijini Dar es salaam, kikionyesha umahiri wao wa wakati wa robo fainali ya shindano la Dance100% lililofanyika katika Viwanja vya Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam .Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 5.
Vijana wa kundi la Tamtamu la Ilala jijini Dar es salaam, wakikonga nyoyo za mashabiki kwenye robo fainali ya shindano la Dance 100% linaloandaliwa na EATV na kudhamiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika Viwanja vya Don Bosco Oysterbay.Kundi litakaloshinda litajinyakulia kitita cha shilingi milioni 5.
Kundi la Dar Crew la Mbagala jijini Dar es salaam, wakishiriki robo fainali ya shindano la Dance100% lililofanyika kwenye Viwanja vya Don Bosco Oysterbay .Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.Mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 5.
Umati wa watu waliofurika kwenye Viwanja vya Don Bosco Oysterbay Dar es Salaam, wakifuatilia mchuano wa robo fainali ya shindano la Dance100% lililoandaliwa na EATV na Kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Kundi la W.T la Temeke la jijini Dar es Salaam,wakikonga nyoyo za mashabiki wakati wa robo fainali ya Shindano la Dance% lilifanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Kikundi cha T.O.P cha Temeke jijini Dar es Salaam,wakiburudisha vilivyo wakati wa robo fainali ya Shindano la Dance% lililofanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.Mshindi ataondoka na kitita cha shilingi Milion 5.
Comments
Post a Comment