MAJANGA ARSENAL! OLIVIER GIROUD AHOFIWA KUUMIA, KUWA NJE YA DIMBA KWA MIEZI MITATU …WENGER HUENDA AKAMSAJILI LOIC REMY
ARSENAL imebaki na bumbuwazi kufuatia mashaka ya kuumia kwa mshambuliaji wake Olivier Giroud ambaye anakwenda kufanyiwa kipimo cha kiwiko chake cha mguu kwa mara ya pili na huenda akalazima kutocheza kwa miezi mitatu
Pengine kocha wa Arsenal, Arsene Wenger atalazimika kubisha hodi tena kwa mshambuliaji wa QPR, Loic Remy kwa pauni milioni 10 au kuachana na mpango wa kumuuza Lukas Podolski kama mashambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa atatakiwa kukaa nje ya dimba kwa muda mrefu.
Giroud, ambaye alipata maumivu ukingoni mwa mchezo wa Ligi Kuuu ulioisha kwa sare ya 2-2 dhidi ya Everton, alionekana kama ataweza kucheza mechi ya kufa na kupona ya mchujo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Besiktas.
Lakini Sportsmail inaamini kuwa nyota huyo wa miaka 27 atashindwa kucheza angalau kwa wiki mbili na kuna hata hofu kuwa mguu wake umevunjika jambo litakalosababisha kuwa nje kwa miezi na siyo wiki kadhaa tena.
Kipimo cha kwanza hakikutoa picha kwa usahihi na sasa anapelekwa kufanya kipimo kwa mara ya pili.
Comments
Post a Comment