NANI kati wa warembo 17 ataibuka kuwa mshindi wa shindano la Redd's Miss Temeke 2014 Ijumaa hii? Jibu litabatikana kwenye viwanja vya TCC Club Chang'ombe jijini Dar es Salaam, sehemu ambayo tukio hilo kubwa litafanyika.
Warembo hao kutoka vitongoji vya Mbagala, Kurasini na Chang'ombe, watapanda jukwaani kuwania taji hilo, ambapo washindi wa tatu watapata tiketi ya kushiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014.
Akizungumza Dar es Salaam, mkurugenzi BMP Promotions inayoaandaa Miss Temeke, Benny Kisaka alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yamekamilika kama yalivyopangwa na wanatarijia kutoa warembo watakao kwenda kunyakua taji la Miss Tanzania.
Kisaka aliwataja Warembo wanaotarajiwa kupanda jukwaani ni Subira Ally, Hellen Yughin, Catherine Alex, Dalina David, Winfrida Guntram, Salama Salehe, Grace John, Lilian Lothy, Amina Salim, Rebecca Mdamu, Sitti Mtemvu, Hellen Sule, Neema Mollel, Lucy Lewis, Esther Mnahi, Pauline Nkini na Patricia Ponsian ambao walikuwa chini ya ukufunzi wa Super Bokilo, Shadya Mohamed na Sweet Remmy.
Alisema mkali wa bongo fleva, Khalid Mohamed TID almaarufu kama Top in Dar, Wanne Star, Makirikiri wa Tanzania, Young Suma, Super Bokilo na wasanii mbalimbali wanatarajia kupamba shoo hiyo ambayo itasindikizwa na Dj John Peter Pantelakis.
Wadhamini wa shindano hilo ni Redds, Zanzi, Michuzi Media Group, Radio EFM 93.7, Cash & Carry Distributors, Kitwe General Traders, Rio Gym & Spa, CXC Africa, 88. 5 Clouds FM, City Sports Lounge, Gazeti la Jambo Leo, Kiwango Security na 100.5 Times FM.
Comments
Post a Comment