|  | 
| Liverpool imeng'ara                            leo kutoka kulia Sturridge, Gerrard na                            Balotelii LIVERPOOL imeichapa mabao 3-0 Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa White Hart Lane.Mabao ya Liverpool yamefungwa na Raheem Sterling dakika ya nane kwa shuti la umbali wa mita saba, Steven Gerrard dakika ya 48 kwa penalti baada ya Eric Dier kumchezea rafu Joe Allen na Alberto Moreno dakika ya 60. | 
Mshambuliaji mpya, Mario Balotelli                  aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan wiki                  iliyopita, leo amecheza mechi yake ya kwanza Liverpool,                  lakini hakufunga licha ya kucheza soka nzuri.
                          Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet,                  Manquillo, Moreno, Gerrard, Lovren, Sakho, Henderson,                  Sterling/Enrique dk86, Sturridge, Balotelli/Markovic                  dk61 na Allen/Can dk61.
                          Tottenham Hotspur: Lloris, Dier,                  Rose/Davies dk72, Capoue, Kaboul, Vertonghen, Lamela,                  Bentaleb/Dembele dk59, Adebayor, Eriksen/Townsend dk59                  na Chadli
                    CHANZO                BIN ZUBERY
        
Comments
Post a Comment