LIVERPOOL YACHARUKA, YAIPIGA TOTTENHAM 3-0 … Alberto Moreno afunga goli la msimu, Balotelli apoteza nafasi nne za wazi
LIVERPOOL imerejea kwenye makali yake baada ya kucheza kandanda safi na kuiadhibu Tottenham 3-0 iliyokuwa uwanja wa nyumbani katika mchezo mkali wa Ligi Kuu ya England.
Kikosi cha Brendan Rodgers kiliidhibiti vilivyo Tottenham na kusukuma mashambulizi makali mwanzo mwisho na kama Liverpool wangetumia vizuri nafasi walizopata basi wangeondoka na kapu la magoli.
Mshambuliaji mpya wa Liverpool Mario Balotteli ambaye alikuwa anacheza mchezo wake wa kwanza, alipoteza nafasi nne za wazi za kufunga mabao kabla hajapumzishwa dakika ya 61.
Rahim Sterling aliyefunga bao la kwanza dakika ya nane, naye pia alipoteza nafasi moja ya wazi.
Kama kuna tukio la kusisimua zaidi ni dakika ya 60 pale beki mpya wa Liverpool, Alberto Moreno alipokimbia kutoka zaidi ya nusu ya uwanja na kuchanja mbuga hadi kwenye 18 ya Tottenham na kufumua shuti kali lililozama wavuni, hilo likiwa na bao la tatu likifuatia lile la pili lililofungwa na nahodha Steven Gerrard daikia ya 49.
Tottenham Hotspur: Lloris, Dier, Rose (Davies 72), Capoue, Kaboul, Vertonghen, Lamela, Bentaleb (Dembele 59), Adebayor, Eriksen (Townsend 59), Chadli.
Liverpool: Mignolet, Manquillo, Moreno, Gerrard, Lovren, Sakho, Henderson, Sterling (Enrique 86), Sturridge, Balotelli (Markovic 61), Allen (Can 61).
Comments
Post a Comment