LIGI YA MABINGWA: LIVERPOOL YAPANGWA NA REAL MADRID ...CITY NA BAYER MUNICH ...ARSENAL NA BORUSSIA

MANCHESTER CITY imepangwa kundi kundi la kifo kwenye michuano ya Champions League kwa kuwekwa kundi moja na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich.

City ambao ni mabingwa wa England wako kundi E pamoja na timu za CSKA Moscow na Roma.

Liverpool wanaorejea Champions League wako kundi B ambapo watakutana na mabingwa watetezi Real Madrid, Basle na Ludogorets.

Arsenal wanaoshiriki hatua ya makundi ya Champions League kwa mwaka wa 17 mfululizo, wamepangwa kundi D na timu za Borussia Dortmund, Galatasaray na Anderlecht.

Makundi kamili ni haya hapa:

KUNDI A: Atletico Madrid, Juventus, Olympiacos, Malmo

 

KUNDI B: Real Madrid, FC Basel, Liverpool, Ludogorets

 

KUNDI C: Benfica, Zenit St Petersburg, Bayer Leverkusen, Monaco

 

KUNDI D: Arsenal, Borussia Dortmund, Galatasaray, Anderlecht

 

KUNDI E: Bayern Munich, Manchester City, CSKA Moscow, Roma

 

KUNDI F: Barcelona, Paris St-Germain, Ajax, APOEL

 

KUNDI G: Chelsea, Schalke, Sporting Lisbon, Maribor

 

KUNDI H: FC Porto, Shakhtar Donetsk, Athletic Bilbao, BATE Borisov

Comments