KAGAWA AKAMILISHA USAJILI WAKE BORUSSIA DORTMUND …asema historia yake na Borussia ilikuwa bado haijakamilika


KAGAWA AKAMILISHA USAJILI WAKE BORUSSIA DORTMUND …asema historia yake na Borussia ilikuwa bado haijakamilika

Return: Borussia Dortmund have re-signed                    midfielder Shinji Kagawa from Manchester United for                    £6.3m

KIUNGO wa Manchester United Shinji Kagawa amekamilisha usajili wa kujiunga na timu yake ya zamani Borussia Dortmund kwa ada inayoripotiwa kufika pauni milioni 12.5.

Borussia Dortmund imetangaza rasmi kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Japan amerejea tena baada ya kukaa Old Trafford kwa miaka miwili.

Kagawa mwenye umri wa miaka 27, ameichezea United mara 57 na kufunga magoli sita ikiwemo hat-trick dhidi ya Norwich, lakini akashindwa kuishashawishi klabu kiuwezo tofauti na vile walivyodhani wakati wakimsaliji.

"Nilisema tangu mwanzo wakati naondoka klabu hii kuwa historia yangu na Borussia Dortmund bado haijakamilika," Kagawa aliuambia mtandao rasmi wa Borussia Dortmund na kuongeza: "Dortmund ni kama familia na nashukuru kuwa hawajanisahau."



Comments