HIKI NDICHO KIKOSI KIPYA CHA ENGLAND … Roy Hodgson adumbukiza makinda wanne


HIKI NDICHO KIKOSI KIPYA CHA ENGLAND … Roy Hodgson adumbukiza makinda wanne

Fresh: Calum Chambers has been named in the England                  squad after an impressive start to his Arsenal career

KOCHA wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson ametaja kikosi chake kipya ndani yake wakiwemo wachezaji wanne ambao hawajawahi kuichezea Englan hata mara moja.

Kikosi hicho ni kwaajili mchezo wa kirafiki dhidi ya Norway pamoja na mchezo wa kufuzu Euro 2016 dhidi ya Switzerland mwezi ujao.

Machipukizi Jack Colback, Calum Chambers, Danny Rose na Fabian Delph wamejumuishwa kwenye kikosi hicho cha wachezaji 22 chenye sura mpya.

Winga wa Tottenham, Andros Townsend amerudishwa kikosini baada ya kukosa michuano ya kombe la dunia kufuatia kuumia kwake. Beki wa Everton John Stones mwenye umri wa miaka 20 naye ni miongoni mwa waliobahatika kuitwa na kocha Roy Hodgson.

Kikosi kamili ni hiki hapa: MAKIPA: Fraser Forster (Southampton), Ben Foster (West Bromwich Albion), Joe Hart (Manchester City)

MABEKI: Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Calum Chambers (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Manchester United), Danny Rose (Tottenham Hotspur), John Stones (Everton)

VIUNGO: Jack Colback (Newcastle United), Fabian Delph (Aston Villa), Jordan Henderson (Liverpool), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Raheem Sterling (Liverpool), Andros Townsend (Tottenham Hotspur), Jack Wilshere (Arsenal)

WASHAMBULIAJI: Rickie Lambert (Liverpool), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Danny Welbeck (Manchester United).



Comments