FM ACADEMIA KUTUA ARUSHA KWA KISHINDO KUZINDUA ALBAMU YAO MPYA SEPTEMBER 5 VIWANJA VYA UKUMBI WA TRIPLE A
 wasanii                wa bendi ya fm Academia wakiwa jukwaani wanaimba wapili                kulia ni Rais wa bendi Nyoshi 
        | Rapa wa bendi ya Fm Academia akiwa anashambulia jukwaa wakati wa shoo. | 
| wanenguaji wa bendi ya Fm wakiwa kazini wote hawa watakuwepo katika uzinduzi huu wa Albamu ya Chuki ya nini usikose ni balaa | 
Fm                 Academia baada ya kukaa kwa muda wa miaka 4 (minne) yaani                kuanzia mwaka 2010 mpaka 2013 sasa wanatarajia kuzindua                rasmi  album mpya kabisa inayojulikana kwa jina la Chuki                ya nini ndani ya jiji la Arusha na vitongoji vyake .
         Album                ya chuki ya nini imebeba nyimbo kumi ndani yake,nazo                ni:-Chuki ya nini, Fataki ,Otilia ,Ndoa ya                kisasa,Neema,Dai chako                ulaumiwe,Maisha,Madudu,Miraessa.album ya chuki ya nini ni                album yenye kiwango cha kimataifa ambapo nyimbo hizi zote                zitazinduliwa rasmi septembar tano mwaka huu ndani ya                viwanja vya  ukumbi wa Triple A jijini Arusha
        Akizungumza                na waandishi  wa habari jijini hapa mkurugenzi wa SB                Intamenti Seif Manyota alisema kuwa bendi hiyo inatarajia                kutua jijini Arusha kwa kishindo kwa ajili ya uzinduzi huu                wa albamu mpya ambapo alibainisha kua tukio hilo litakuwa                la kihistoria.
        Alisema                kuwa  hii ni mara ya kwanza kwa bendi hii  kuzindua                albamu  nje ya mkoa wa dar es salaam na kwa hivyo wameamua                kuwapa heshima kubwa wapenzi wa bendi hiyo wa mkoa wa                Arusha  pamoja na mikoa ya kanda ya kaskazini kwa ujumla                hii ikiwa ni heshima ya kipekee.
        "uzinduzi                huu wa  albamu sio tu tunazindua  nyimbo mpya bali                tunazindua pia vyombo vipya na staili mpya za kuicheza                gwasuma kama vile mnavyojua bendi ya fm  ni wazee wa pamba                wazee wa kushambulia jukwaa"alisema Manyota
        Aidha                alibainisha kuwa kwa mkoa wa Arusha wameamua kuwapa                kipaumbele na pia kwakuwa kunawapenzi wengi wa ngwasuma                wameamua kufanya shoo hii nje ambapo ,kutafugwa jukwaa la                kisasa  kabisa.
        Alitaja                baadhi ya nyimbo ambazo zipo katika albamu ambayo                inazinduliwa kuwa ni pamoja na Chuki ya nini,ndoa ya                kisasa fataki  pamoja na nyinginezo.
        Aidha                kwa upande  mungine alisema uzinduzi huu autaishia Arusha                tu bali wakazi wa Moshi na Tanga nao watapata burudani hii                na kuzitambua staili mpya pamoja na nyimbo mpya zilizopo                kwenye albamu hii.
        Alisema                kua pia kutakuwa na CD na DVD za albamu hiyo mpya                iliyozinduliwa huku akisema kuwa kwa upande wa Arusha                kiingili    akuwa 20000 na unapatiwa CD moja buru                mlangoni.
        kwa                upande wa Rais wa bendi hiyo Nyoshi alisema kuwa timu                 yake yote imejipanga vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi                wa Arusha  na kuwapa staili mpya ikiwemo ile ya vundesa                 ambapo alisema kuwa wameiboresha na imekuwa ya kiufasaha                 zaidi  na ina vinjonjo vingi zaidi ,staili tamu  pamoja na                maneno matamu.
        
        Alisema                kuwa lengola kubwa la kuzindua albaimu hii apa jijini                Arusha ni pamoja na kuwaelewesha wapenzi wao nyimbo mpya                na kuakikisha wapenzi wao wanajua staili zao zote za                 nyimbo hizo na  sio ivyo tu pia alisema kuwa kwa kipindi                 hiki wanataka kuwa wakazi wa arusha zawadi ya kuwaletea                wasanii wote wa bendi hiyo ambapo alisema wapo 32  na wote                watafika jijini Arusha
        
Comments
Post a Comment