FERNANDO TORRES NJIANI KUTIMKIA AC MILAN

MSHAMBULIAJI wa Fernando Torres yuko mbioni kwenda AC Milan na tayari wakala wake yupo kwenye maongezi na Chelsea kwaajili ya uhamisho  huo.

AC imedhamiria kutafuta mbadala wa Mario Balotelli aliyejiunga na Liverpool ambapo makamu wa rais wa klabu hiyo Adriano Galliani amesema: “Lengo letu ni kuchukua mshambuliaji bora. Fernando Torres? Ndio ni mshambuliaji bora. Wacha tuone kama ni yeye atakayekuja au mwingine yeyote yule.”

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho anataka kumtema Torres ili aweze kusajili mshambuliaji mwingine kabla dirisha la usajili halijafungwa.

Torres amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake unaomwingizia pauni 150,000 kwa wiki hapo Stamford Bridge, lakini anataka alipwe mshahara wake wote wa miaka miwili kwa mkupuo ili aweze kuondoka Chelsea.

Comments