FAINALI YA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) KUFANYIKA TAREHE 30 AUGUST 2014 NDANI YA UKUMBI WA MLIMANI CITY

 Mc Pilipili Akiongea mbele ya                Waandishi wa habari wakati wa Mkutano na Waandishi wa                habari kuhusiana na fainali kubwa ya Shindano la Tanzania                Movie Talents (TMT) litakalofanyika tarehe 30 August 2014                katika Ukumbi wa Mlimani City kuanzia Mida ya Saa 7:30 PM                (Usiku) huku viingilio vikiwa ni Elfu Hamsini (50,000/=)                kwa V.I.P na Elfu thelethini (30,000/=) kwa Kawaida.                Wapili Kushoto ni Meneja Mradi TMT Joshua Moshi, Julieth                Samson "Kemmy" ambae ni Mwalimu wa Nidhamu na Afisa                Uhusiano TMT, Josephat Lukaza.
           Washiriki kumi bora Ambao                wameingia kwenye fainali ya Kuwania Shilingi Milioni 50 za                kitanzania ambayo fainali itafanyika tarehe 30 August 2014                katika Ukumbi wa Mlimani City  huku viingilio vikiwa ni                Elfu Hamsini (50,000/=) kwa V.I.P na Elfu thelethini                (30,000/=) kwa Kawaida.
            
           Mmoja wa washiriki walioingia                Kwenye fainali ya TMT, Mwanaafa Mwinzago akiongea na                waandishi wa habari leo wakati wa mkutano uliofanyika                katika Ofisi za Proin zilizopo Mikocheni.
          Baadhi ya washiriki na waandishi                wa habari waliofika katika mkutano na waandishi wa habari                uliofanyika leo katika ofisi za Proin zilizopo Mikocheni.
          BAADA ya mchakato wa                kuzunguka mikoani kwa ajili ya kusaka wasanii wenye vipaji                vya uigizaji, hatimaye fainali za Tanzania Movie Talents                 ( TMT) zitafanyika  Jumamosi ya Agosti 30 mwaka huu                 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
          Mshindi wa shindano hilo                atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 50 wakati                burudani itadondondoshwa  na Christian Bella na                mchekeshaji MC Pilipili.
        
Comments
Post a Comment