Exclusive: Mtanzania DABO ametajwa kuwania tuzo za reggae za kimataifa na muziki wa dunia 2014 (IRAWMA)
Unaweza kuwa humfahamu kwa vile hana kelele nyingi....TUONYESHE UZALENDO KWA KUMPIGIA KURA SASA.
Msanii bora wa muziki wa Reggae Tanzania, DABO (Pichani) amepata nafasi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania katika anga za kimataifa, baada ya kuchaguliwa kuwania tuzo kubwa kabisa za reggae za kimataifa na muziki wa dunia 2014 (International Reggae and World Music Awards (IRAWMA).
DABO anawania tuzo hizi katika kipengele cha Mtumbuizaji Mpya Bora, akikabiliwa na ushindani kutoka kwa wasanii MC Norman kutoka Uganda, Alkaline na Kranium kutoka Jamaica na Shatta Wale kutoka Ghana.
Zoezi la kuwapigia kura wasanii hawa kuwawezesha kushinda linaendelea sasa mtandaoni. Link ya kumpigia kura ni: http://www.irawma.com/irawma_vote2014
DABO ametajwa kuwania kipengele cha Best New Entertainer
Kwenye kipengele hicho, DABO anachuana na
* Daniel Bambatta Marley - Jamaica
* MC Norman - Uganda, Africa
* Alkaline - Jamaica
* Kranium - Jamaica
* Shatta Wale – Ghana
Asante kwa Kuunga mkono zoezi zima ndio kama linaanza!
Comments
Post a Comment