Emmanuel Okwi atua Msimbazi kwa mkataba wa miaka miwili, Asema Yanga Wamemuacha

Emmanuel Okwi kusaini mkataba usiku huu mkataba wa miaka miwili Simba.

“Yanga wameniacha, nikachukua uamuzi wa kurudi Simba na kuomba kuichezea nao wamenikublia.

“Najua Yanga wamenishitaki TFF au Fifa, nitaendelea kulishughulikia suala hilo wakati nikiwa naitumikia Simba.

“Nashukuru kwa kuwa wamenipokea kwa mikono miwili,” alisema Okwi akionyesha kujiamini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema wamemchukua Okwi baada ya kuandika barua kuomba arudi.

“Tumempokea baada kuipokea barua yake na kuijadili, kwa kuwa Yanga wamemuacha na hata FIfa inasisitiza wachezaji kupata nafasi ya kucheza ili kuepusha kuua vipaji vyao, tumeamua kuwa naye,” alisema Hans Poppe. 

Baada ya kumpokea kwa mikono miwili, Simba imeamua kumrudishia Emmanuel Okwi jezi yake namba 25.

Kabla ya kuondoka kwenda Etoile du Sahel alipouzwa 'bure' na Simba chini ya Ismail Aden Rage, Okwi alikuwa akitumia jezi hiyo

Yanga pia walimpa jezi hiyo, lakini leo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amethibitisha kuwa Simba imempa Okwi namna 25.

Baada ya kupokea namba hiyo, Okwi kesho anapaa Zanzibar kuungana na wenzake ambao wako kambini kujiandaa na Ligi Kuu Bara.

Comments