ANGEL DI MARIA amefichua kuwa mchezaji mwenzake wa zamani katika Real Madrid Cristiano Ronaldo, alimwambia avae jezi namba 7 pindi atakaposaini Manchester United.
Di Maria ambaye amesani mkataba wa miaka mitano kwa mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki, amekabidhiwa jezi hiyo yenye mvuto wa kipekee Old Trafford, ikiwa imevaliwa na masupastaa kama Ronaldo, Eric Cantona na David Beckham.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina alitambulishwa rasmi United katika mkutano wa waandishi wa habari Alhamisi na kufichua ni jinsi gani Ronaldo alimtaka avae jezi hiyo.
“Cristiano aliniambia ni namna gani jezi namba 7 ina maana kubwa. Nilitaka kuvaa jezi hii. Klabu pia imetaka nivae jezi namba 7,” alisema Di Maria.
Comments
Post a Comment