DI MARIA ASAINI MIAKA MITANO OLD TRAFFORD NA KUSEMA HAKUNA KLABU NYINGINE YOYOTE AMBAYO INGEMFANYA AACHANE NA REAL MADRID ZAIDI YA MANCHESTER UNITED
ANGEL DI MARIA hatimaye amekuwa mchezaji wa Manchester United kwa rekodi ya manunuzi Uingereza - pauni milioni 59.7 na kusema asingeweza kuiacha Real Madrid kwa klabu nyingine yoyote ile isipokuwa Manchester United.
Winga huyo wa Argentina amesaini mkataba wa miaka mitano Old Trafford na ataingiza pauni milioni 6.5 kwa mwaka baada ya kukatwa kodi. Kipato kitakachomfanya nyota huyo wa miaka 26 awe mchezaji wa pili wa United anayelipwa pesa nyingi zaidi nyuma ya Wayne Rooney.
Kauli ya Di Maria kwamba angeeicha Real Madrid kwa ajili ya United pekee, itawakera Manchster City. Mabingwa hao wa watetezi wa Barclays Premier League walimpa ofa kama hiyo Di Maria wiki iliyopita.
"Hakika nina furaha kujiunga na Manchester United," alisema Di Maria.
"Nimekuwa nikifurahia muda wangu Hispania na vilabu vingi vilivutiwa nami, lakini United ni klabu pekee ya kunifanya niachane na Real Madrid," alisema Di Maria.
Comments
Post a Comment