DI MARIA AKARIBIA KUTUA MANCHESTER UNITED …jezi namba 7 yamsubiri



DI MARIA AKARIBIA KUTUA MANCHESTER UNITED …jezi namba 7 yamsubiri

Action man: Angel Di Maria featuring for Real                    Madrid against Atletico Madrid in their Super Cup                    clash

MANCHESTER United inakaribia kumnasa Angel Di Maria baada ya nyota huyo wa Real Madrid kuchagua kwenda Old Trafford, hii ni kwa mujibu wa ripoti za vyombo kadhaa vya habari vya Hispania na England.

Gazeti la maarafu la Hispania Marca limesema Di Maria ataigharimu United kiasi cha pauni milioni 56 na kwamba dili hilo liko ukingoni kukamilika.

Huko England Sky Sports inaripoti kuwa Di Maria amechagua kwenda Old Trafford licha ya ushawishi kutoka Paris Saint-Germain ya Ufaransa na kwamba atavishwa jezi namba 7 iliyovaliwa na msataa kama Cristiano Ronaldo, David Beckham, Eric Cantona na George Best.



Comments