USAJILI wa pauni wa milioni 59.7 wa Angel Di Maria kutoka Real Madrid kwenda Manchester United ni kama umekamilika baada ya nyota huyo kufaulu vipimo vya afya.
Dili hilo linalotegemewa kuvunja rekodi ya manunuzi England, litamshuhudia Di Maria akiingiza pauni 200,000 kwa wiki katika mkataba wake wa miaka mitano.
Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina aliruka kwenda Manchester Jumatatu ambapo wakala wake Jorge Mendes alipigwa picha Jumanne mchana akiwa kwenye gari la kocha wa United Louis van Gaal.
Van Gaal alionekana mwenye furaha akiwa na Mendes kuelekea Aon Training Complex kukamilisha dili la kumleta Di Maria Old Trafford.
Di Maria ataungana na wachezaji wenzake mazoezini siku ya Alhamisi na klabu inategemewa kukamilisha hati yake ya kufanya kazi England Ijumaa mchana ili aweze kucheza dhidi ya Burnley Jumamosi.
Comments
Post a Comment