CHELSEA YAIPIGA BAO ARSENAL …Loic Remy asani miaka minne Stamford Bridge, asema amefuata mataji



Transfer: Loic Remy has signed for Chelsea on a                  four-year deal after the Blues met his buyout clause

CHELSEA imeshinda vita dhidi ya Arsenal katika kusaka saini ya mshambuliaji Loic Remy wa QPR na kumsainisha mkataba wa miaka minne kukipiga Stamford Bridge.

Wawakilishi wa Loic Remy tayari walikuwa wamefikia pazuri na Chelsea kimaongezi kabla Arsenal haijatia mguu kutaka kuteka nyara dili hilo.

Mchezaji huyo wa zamani wa Marseille ameiambia wesite ya Chelsea: "Najiskia furaha na fahari. Nilipoambiwa Chelsea inanitaka nikasema 'wache niende' kwa sababu ni moja klabu bora duniani.

"Najiskia fahari na furaha kujiunga na Chelsea leo. Kwangu mimi ni jambo kubwa. Nina kiu kubwa ya kuungana na wachezaji wenzangu na kucheza mchezo wangu wa kwanza hapa.

"Nakumbuka msisimko wa kuvutia Stamford Bridge wakati nilipocheza mara ya kwanza pale nikiwa na Marseille na nashindwa kuvumilia kusubiri siku ya kucheza kwa mara ya kwanza mbele ya mashabiki wangu wapya.

"Niko hapoa kwaajili ya kusaka maendeleo. Nina nafasi sasa ya kupata kilicho bora kupitia timu hii. Nahitaji kushinda mataji. Hii ndiyo sababu kwanini nimesaini Chelsea."

Remy: 'When I heard Chelsea wanted me I said                  "let's go" because they are one of the best                  clubs in the world.'

Loic Remy ilikuwa asaini Liverpool wiki kadhaa zilizopita lakini timu hiyo ikamtosa dakika za mwisho kwa kusema mshambuliaji huyo amefeli vipimo vya afya.

Lakini kocha wa Chelsea Jose Mourinho amedai amehakikishiwa kuwa mshambuliaji huyo hana tatizo la kiafya litakaloathiri uchezaji wake.



Comments