CHELSEA SPIDI 120, DIEGO COSTA MOTO CHINI …Everton waiosoma namba …pata matokeo ya mechi zote za Jumamosi
CHELSEA imezidi kutimua vumbi kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kuifumua Everton kwa bao 6-3.
Ilikuwa ni mechi ya aina yake ya funga ni kufunga, lakini mwisho wa siku timu makini yenye wachezaji makini ikaibuka kuwa mshindi.
Mshambuliaji mpya wa Chelsea Diego Costa ameendelea kucheka na nyavu katika kila mechi lakini safari hii ameongeza dozi.
Costa akatupia wavuni mabao mawili – goli la kwanza likiwa limetinga dakika ya kwanza ya mchezo na bao la mwisho alilofunga dakika ya 90.
Magoli mengine ya Chelsea yalifungwa na Branislav Ivanovic dakika ya 3, goli la kujifunga la Seamus Coleman dakika ya 67 na Nemanja Matic dakika ya 74.
Everton walipata magoli yao kupitia kwa Kevin Mirallas dakika ya 45, Steven Naismith dakika ya 69 na Samuel Eto'o dakika ya 76.
Everton: Howard, Coleman, Jagielka, Distin, Baines, McCarthy, Barry, Mirallas, Naismith, McGeady (Eto'o 70), Lukaku (Besic 89).
Chelsea: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Matic,Willian (Mikel 75),Fabregas (Drogba 89),Hazard (Luis 83), Costa.
Matokeo ya mechi zote za Ligi Kuu zilizochezwa Jumamosi ni:
Burnley 0 - 0 Manchester United
Manchester City 0 - 1 Stoke City
Newcastle United 3 - 3 Crystal Palace
Queens Park Rangers 1 - 0 Sunderland
Swansea City 3 - 0 West Bromwich Albion
West Ham United 1 - 3 Southampton
Everton 3 - 6 Chelsea
Comments
Post a Comment