CHELSEA inatimua vumbi kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kuinyuka Leicester City 2-0 na kujikusanyia pointi 6 safi, hii ikiwa ni baada ya kuvuna ushindi wa 3-1 dhidi Bunrley katika mchezo wa kwanza.
Hadi mapumziko, Chelsea iliyokuwa nyumbani ilibanwa mbavu na kushidwa kugusa nyavu za Leicester City lakini ikacharuka kipindi cha pili na kutupia mipira wavuni mara mbili.
Alianza mshambuliaji mpya Diego Costa aliyefungua milango kwa bao la dakika ya 63, hili likiwa goli lake la pili kwenye Ligi Kuu.
Eden Hazard akaihakikishia ushindi Chelsea kwa kufunga bao la pili dakika ya 77.
CHELSEA: Courtois 8, Ivanovic 7, Cahill 6, Terry 6, Azpilicueta 6.5, Matic 6, Fabregas 7, Oscar 7 (Willian 6, 70), Hazard 6.5, Schurrle 6.5 (Ramires 6.5, 64), Costa 7 (Drogba 6.5, 80).
LEICESTER CITY: Schmeichel 8.5, De Laet 7, Konchesky 6.5, Morgan 6.5, Hammond 8 (Taylor-Fletcher 6.5, 73), King 6.5, Schlupp 7, Mahrez 7.5 (Albrighton 6, 68), Nugent 7, Ulloa 6.5 (Wood 84).
Comments
Post a Comment