CARLO ANCELOTTI ASEMA SAMI KHEDIRA HAENDI POPOTE … Arsenal, Chelsea na Manchester United walie tu


CARLO ANCELOTTI ASEMA SAMI KHEDIRA HAENDI POPOTE … Arsenal, Chelsea na Manchester United walie tu

man utd, arsenal, chelsea, sami khedira

 CARLO ANCELOTTI amesema kiungo wake Sami Khedira atabakia Real Madrid msimu huu, kauli ambayo itazinyong'onyeza timu nyingi za England.

Wapinzani wakubwa wa Premier League Arsenal, Chelsea na Manchester United walikuwa wakihusishwa kwa kiasi kikubwa na uhamisho wa kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani.

Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari, kocha huyo wa Real Madrid akazima uvumi huo kwa kusema: "Khedira ana furaha kuwa nasi na hataondoka. Utata wake umeshamalizwa na sasa atabakia Real Madrid."



Comments