BAYERN MUNICH YAZIPIGA BAO MAN UNITED, MAN CITY NA CHELSEA …yamsajili sentahafu Mehdi Benatia wa Roma



BAYERN MUNICH YAZIPIGA BAO MAN UNITED, MAN CITY NA CHELSEA …yamsajili sentahafu Mehdi Benatia wa Roma

Main man: Manchester City, Manchester United and                    Chelsea were all interested in the Moroccan defender

MABINGWA wa Ujerumani Bayern Munich wameshinda mbio za kumsaka beki wa hali ya juu Mehdi Benatia kutoka Roma.

Sentahafu huyo wa kimataifa wa Morocco mwenye umri wa miaka 27 alikuwa pia akiwaniwa na Manchester City, Manchester United na Chelsea baada ya kuisaidia Roma kushika nafasi ya pili Serie A msimu uliopita.

Lakini ni Bayern Munich iliyofanikiwa kupata saini ya mchezaji huyo anayetarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano kwa ada ambayo imefanywa siri na klabu zote mbili.

Taarifa ya Bayern Munich imesema: "Benatia atawasili Munich siku chache zijazo kwaajili ya kufanya vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wa miaka mitano."



Comments