AUDIO: KUWA WA KWANZA KUSIKILIZA WIMBO MPYA WA TWANGA PEPETA - GANDA LA MUA UTUNZI WAKE SALEH KUPAZA …isikilize rap ya Kantangaze live!
HUU ni wimbo mpya kabisa wa Twanga Pepeta, umepewa jina la "Ganda la Mua" ambao bila shaka yoyote ile utawashika watu ipasavyo.
Ni wimbo bab kubwa, utunzi wake Saleh Kupaza, kazi imefanywa katika studio ya Fleva Ink chini ya producer mwalikwa Said Comorien. Fleva Ink inamilikiwa na Aset.
Katika wimbo huu ambao ndani yake kuna vionjo vya hip hop pamoja na vile vya kiasili, kuna ingizo jipya kabisa katika sauti zitakazosikika – ni sauti ya Rama Pentagone ambaye anarekodi na Twanga Pepeta kwa mara ya kwanza tangu alipojiunga na bendi hiyo mwaka jana akitokea Extra Bongo.
Lakini hayupo Pentagone peke yake, yupo pia rapa Frank Kabatano aliyejumuishwa kundini hivi karibuni akiwa ametokea TO T Band aliyoitumikia kwa miezi michache baada ya kuondolewa Extra Bongo.
Funga kazi ni marejeo ya rapa Msafiri Diouf anayeshuka na rap yake kali ya Kantangaze.
Usikilize hapo chini.
Comments
Post a Comment