ALEX SONG AENDA WEST HAM



ALEX SONG AENDA WEST HAM

West Ham wamemsajili kiungo wa zamani wa Arsenal, Alex Song, 26, kwa mkopo kutoka Barcelona. Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Cameroon, ametambulishwa mbele ya mashabiki kabla ya mchezo dhidi ya Southampton.
"Nadhani klabu hii ina mwelekeo mzuri, na pengine tunaweza hata kumaliza katika nafasi za kucheza makombe ya Ulaya," amesema.
Song alijiunga na Barcelona mwaka 2012 kutoka Arsenal kwa pauni takriban milioni 15.


Comments