KWA mujibu wa ripoti kutoka Italia kiungo wa Juventus na Chile Arturo Vidal (pichani kushoto) amefutilia mbali uwezekano wa yeye kujiunga na Manchester United.
Kwa muda mrefu Vidal alikuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa na safari ya kwenda Old Trafford ambapo kocha wa Manchester United Louis van Gaal aliidhinisha klabu yake kumsaliji kiungo huyo mkabaji.
Real Madrid nayo ni miongoni mwa vilabu vikubwa vinavyotajwa kuwania huduma ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 27.
Lakini alipooulizwa kuhusu hatma yake, Vidal alisema: "Siendi Manchester United."
Vidal tayari amerejea Italia na alipoulizwa na waandishi wa habari iwapo atabakia Juventus, alisema: "Siendi Manchester United. Naweza kusema nitabakia Juventus? Hapana sina uhakika.
"Sina uhakika na hatma yangu Juventus, nitazungumza na Allegri Jumatatu na tutaona kitakachotokea. Sijazungumza na Allegri wala mchezaji mwenzangu yeyote, lakini siendi Manchester United."
Comments
Post a Comment