VAN GAAL ASEMA BORA KUMSUBIRI KEVIN STROOTMAN HADI JANUARI KULIKO KUNUNUA VIUNGO WACHOVU DIRISHA HILI LA USAJILI …adai yupo tayari kuanza msimu na viungo waliopo klabuni
LOUIS van Gaal ameiambia Manchester United kuwa yupo tayari kusubiri hadi dirisha dogo la usajili (mwezi Januari) ili kumsajili kiungo Kevin Strootman kuliko kusajili viungo wachovu dirisha la kiangazi.
Kocha huyo wa United ni shabiki mkubwa wa Strootman na klabu itaendelea kufuatilia maendeleo ya kiungo huyo wa Roma ambaye yuko nje ya dimba kufuatia kuumia kwake vibaya goti.
Van Gaal amekielezea kikosi cha United kwamba hakina uwiano wa kutosha na angependelea kusajili kiungo mkabaji lakini yuko na amani kusubiri hadi Januari ili kumnasa mchezaji huyo wa hali ya juu amabaye ni chaguo lake kuu.
Kocha huyo ameionya United isifanye manunuzi ya pupa na kwamba yuko na furaha ya kufanya kazi na viungo waliopo. Hiyo inamaanisha kuwa Tom Cleverley anaweza akapewa jukumu kubwa kuliko ilivyotegemewa na wengi.
Van Gaal alifanya kazi kwa ukaribu sana na Strootman, 24, wakati alipokuwa akiifundisha Holland na anaamini ni aina ya mchezaji atakayeendana na staili ya soka anayotarajia kuitumia Manchester United.
Comments
Post a Comment