| 
 
 
 
 TIMU ya                    soka ya Waendesha pikipiki maarufu kwa jina la                    Bodaboda ya Uyole imeibuka kidedea katika fainali ya                    Kombe la Bodaboda dhidi ya timu ya Kabwe katika kipute                    kilichopigwa juzi katika uwanja wa Shule ya Msingi                    Mwenge Soweto jijini Mbeya. 
 Katika                    fainali hizo ambazo zimedhaminiwa na Kampuni ya                    vinywaji baridi ya Cocacola Kwanza Mbeya, Mgeni rasmi                    alikuwa ni Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harisson Mwakyembe                    aliyekabidhi zawadi mbali mbali kwa washindi. 
 Timu ya                    Uyole aliibuka kidedea baada ya kuwafunga timu ya                    Kabwe kwa magoli mawili kwa nunge magoli                    yaliyopatikana kupitia kwa Miraji Juma aliyefunga goli                    dakika ya 41 kipindi cha Kwanza baada ya piga ni                    kupige katika lango la Kabwe. 
 Baraka                    Agogo aliandikia goli la pili na la ushindi timu yake                    ya Uyole baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa timu ya                    Kabwe dakika ya 75 na kufanya hadi mwisho wa mchezo                    Uyole 2 na Kabwe 0 katika mpambano ulioamuliwa na                    Mwamuzi Ngole Mwangole. 
 Awali                    katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu                    ulizikutanisha timu za Soweto na Iyunga ambapo timu ya                    Iyunga ilijinyakuliwa nafasi ya Msindi wa tatu baada                    ya kuifunga timu ya Soweto magoli matatu kwa bila. 
 Magoli ya                    timu ya Iyunga yalifungwa na Salim Mvungi dakika ya                    30, na magoli mawili yakifungwa na mshambuliaji hatari                    Pinto Iman katika dakika za 70 na 76 na kuwaacha                    wapinzani wao wakiishia katika nafasi ya nne hadi                    kipenga cha mwisho kilichopulizwa na mwamuzi Kefa                    Kayombo. 
 Ligi hiyo                    iliyoandaliwa na kampuni ya City Sign Promotion &                    marketing Agency ya jijini Mbeya ilianza kutimua vumbi                    Juni 14, Mwaka huu baada ya kufunguliwa na Waziri                    Mwakyembe kabla ya kuifunga tena Julai 26, Mwaka huu. 
 Dk.                    Mwakyembe alikabidhi zawadi kwa washindi ambapo                    mshindi wa Kwanza ambao ni timu ya Uyole alikabidhiwa                    Kombe pamoja na mfano wa Hundi yenye thamani ya                    shilingi Milion mbili kwa ajili ya ununuzi wa Pikipiki                    mpya aina ya Boxer, pamoja na mpira mmoja. 
 Mshindi                    wa pili timu ya Kabwe ilikabidhiwa mfano wa Hundi                    yenye thamani ya shilingi lai saba(700,000) pamoja na                    mpira mmoja huku mshindi wa tatu timu ya Iyunga                    ikikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi                    Laki tatu(300,000) pamoja na mpira mmoja huku mshindi                    wa nne  timu ya Soweto ikiambulia mpira mmoja. 
 Aidha Dk.                    Mwakyembe pia alikabidhi zawadi kwa mfungaji bora                    ambaye alikuwa ni Emanuel Luole kutoka Timu ya Stendi                    ya Umalila Mbalizi aliyejinyakuliwa mfano ya hundi ya                    shilingi laki moja baada ya kufikisha magoli saba,                    Goli kipa bora alitoka tiku ya Kabwe Zakaria Lugano                    aliyepata Shilingi Laki Moja pamoja na timu yenye                    nidhamu ambayo ni Ilomba iliyojipatia shilingi laki                    moja. 
 Hata                    hivyo Waziri Mwakyembe baada ya kumaliza kukabidhi                    zawadi zilizotolewa na wadhamni ambao ni Kampuni ya                    Cocacola pia alijitolea zawadi kwa ajili ya mwamuzi                    bora na mshika kibendera bora ambao aliwapa shilingi                    laki moja kila mmoja. 
 Wakati                    huo huo Waziri Mwakyembe alitimiza ahadi yake kwa                    chama cha Waendesha bodaboda Mkoa wa Mbeya kwa                    kuwakabidhi pikipiki mbili mpya pamoja na jezi mbili                    za mpira wa miguu kwa ajili ya timu ya jiji itayoundwa                    baada ya kumaliza ligi hiyo. 
 Mwisho. 
 Na                      Mbeya yetu 
 
 | 
Comments
Post a Comment