TWANGA PEPETA YAMNYAKUA DANSA MWINGINE WA EXTRA BONGO …ni Dogo White – Hamza Mapande

TWANGA PEPETA YAMNYAKUA DANSA MWINGINE WA EXTRA BONGO …ni Dogo White – Hamza Mapande
TWANGA PEPETA YAMNYAKUA DANSA MWINGINE WA EXTRA BONGO …ni            Dogo White – Hamza Mapande

BENDI ya The African Stars "Twanga Pepeta" imezidi kuimarisha safu yake ya unenguaji baada ya kunyakua dansa wa kiume Hamza Mapande "Dogo White" kutoka Extra Bongo.

Mapande anaungana na madansa watatu waliotimuliwa Extra Bongo, Danger Boy, Maria na Sabrina ambao pia wamechukuliwa na Twanga Pepeta.

Kwa pamoja madansa hao watatambulishwa siku ya Idd Mosi katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni.

Mapende ameimbia Saluti5 kuwa hana tatizo lolote na Extra Bongo na ameagana vizuri na uongozi wa bendi hiyo.

"Nimeingia Twanga Pepeta ili kutafuta changamoto mpya na sikuwa na tatizo lolote na Extra Bongo, nimeishi nao vizuri na najivunia nilichojifunza kutoka kwao," alisema Mapande.

Mapande (pichani juu) ambaye pia aliwahi pia kuwa dansa wa Mchinga Generation, ameitumika Extra Bongo kwa miaka mitatu.

Comments