THE African Stars "Twanga Pepeta" na FM Academia "Wazee wa Ngwasuma" leo watakuwa wakicheza viwanja vya jirani katika maonyesho yao ya Idd Mosi.
Wakati Twanga Pepeta watakuwa Mango Garden Kinondoni wakitambulisha nyimbo mpya na wasanii wapya, FM Academia watakuwa ndani ya ukumbi wa New Msasani Club ulioko Kinondoni Drive in.
Wakati Twanga Pepeta walisimamisha maonyesho yao mwezi wa Ramadhan, FM wao waliendelea na makamuzi kama kawaida japo wiki iliyopita walisimamisha show zao kufuatia msiba wa mwimbaji wao Digital aliyezikwa jana huko kwao nchini Congo DRC.
Twanga Pepeta na FM Academia kwa muda mrefu zimekuwa ni bendi shindani huenda leo zikawa na kazi kubwa ya kuporana mashabiki kutokana na ukaribu wa kumbi hizo
Comments
Post a Comment