KIUNGO wa Atletico Madrid Raul Garcia amesema Fernando Torres atakaribishwa kwa mikono miwili kwa mabingwa hao wa Hispania iwapo ataondoka Chelsea na kurejea nyumbani.
Torres amekuwa akihusishwa na kurejea tena Atletico, sehemu ambayo mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania alichanua vilivyo kabla hajajiunga na Liverpool mwakwa 2007.
Licha kushindwa kuonyesha makali yake ya Liverpool tangu aliopotua Chelsea kwa pauni milioni 50 Januari 2011, Garcia anaamini Torres mwenye umri wa miaka 30 atafiti vizuri Atlectio.
Chelsea tayari imemyakua mshambuliaji Diego Costa na beki Filipe Luis, wote kutoka Atletico kwa jumla ya pauni milioni 48 huku ikimchukua pia kipa wake Thibaut Courtois aliyekuwa akiichezea Atletico kwa mkopo. Hali hii inafanya kuwe na uwezekano mkubwa wa Torres kwenda upande wa pili.
Comments
Post a Comment