KAMA unadhani makali ya msanii wa kizazi kipya TID yamepungua basi unajidanganya, jamaa bado yuko juu kinoma ambapo siku ya Idd Pili aliangusha bonge la show lililofanyika ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala.
Onyesho hilo lililopewa jina la "Usiku wa Mnyama" lilihudhuriwa na mashabiki wengi huku wakifurahia nyimbo za TID hadi kufikia hatua ya kumbeba juu kwa juu.
Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Khalid Mohammed 'TID Mnyama' akizikonga nyoyo za mashabiki wa Dar Live katika Usiku wa Mnyama na Wanyama.
Mnyama TID akijiachia kwa mashabiki wake wa Dar Live.
Mwanamuziki Jafarai akipagawisha mashabiki waliofurika katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.
Jay Moe akifanya makamuzi katika steji ya kupanda na kushuka ya Dar Live.
Inspector Haroun akiwapa hi mashabiki wake ndani ya Dar Live.
Mwanadada Naaziz kutoka Kenya akilishambulia jukwaa la Dar Live.
Masai Sharo akifanya vitu vyake stejini.
Mashabiki wakijiachia kijanja ndani ya Dar Live.
TID akitunzwa Cheni na shabiki wake.
TID akifanya manjonjo yake mbele ya Naaziz.
Nyomi ikifuatilia burudani za Idd Pili ndani ya Dar Live.
(PICHA NA RICHARD BUKOS NA GABRIEL NG'OSHA / GPL)
Comments
Post a Comment