TALENT BAND YA HUSSEIN JUMBE IKO MWANZA IDD MOSI …TOT BAND NDANI YA TABATA

TALENT BAND YA HUSSEIN JUMBE IKO MWANZA IDD MOSI …TOT BAND NDANI YA TABATA
TALENT BAND YA HUSSEIN JUMBE IKO MWANZA IDD MOSI …TOT            BAND NDANI YA TABATA

KUNDI la Talent Band linaloongozwa na Hussein Jumbe litafanya maonyesho mawili ya Idd Mosi na Idd Pili ndani ya jiji la Mwanza.

Hussein Jumbe ameiambia Saluti5 kuwa bendi yake itatumbuiza ndani ya ukumbi wa River Side Park Hotel eneo la maduka mawili kwa siku mbili mfululizo Idd Mosi na Idd Pili.

Nalo kundi la TOT Band chini Redock Mauzo na Kabatano litafanya maonyesho yao ya Idd Mosi na Idd Pili katika ukumbi wa Kwa Swai Bar ulioko Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam.

Kiongozi wa TOT Band "Vijana Fashion", Redock Mauzo ameieleza Saluti5 kuwa maonyesho yao yataanza saa 1 jioni na kuendelea.

Comments