SIMANZI ZAENDELEA KUTAWALA NDANI YA NYUMBA YA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) MARA BAADA YA MSHIRIKI MWINGINE KUAGA SHINDANO



Majaji wa shindano la TMT wakimsikiliza kwa makini Mshiriki wa TMT, Mwanaafa Mwinzago (anayeonekana kwenye runinga mbele) wakati akijielezea kabla ya filamu fupi aliyoshiriki kuonyeshwa ili majaji waweze kutoa hukumu kwa washiriki wa kundi hilo
 Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) katikati wakiwasikiliza washiriki wa kundi la kwanza wanavyojielezea kabla ya filamu fupi waliyochezwa kuonyeshwa katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wiki iliyopita
 Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiangalia filamu fupi iliyochezwa na washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) katika ukumbi wa makumbusho kabla ya kuanza kutoa hukumu kwa washiriki ni nani anatoka na nani anabaki.
Jaji Vyonne Cherry au Monalisa akitoa maoni kwa washiriki waliokuwa wameshiriki kwenye filamu fupi iliyochezwa na washiriki wa TMT
  Kundi la Kwanza la Washiriki wa TMT waliocheza filamu fupi iitwayo LUGHA GONGANA wakiwa mbele ya meza ya Pilato katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa mwanzoni mwa wiki.
 Mshiriki wa TMT, Mwanaafa Mwinzago akifunika uso wake kwa kutoamini kuwa ameponea kwenye tundu la sindano kutokana na kuondolewa katika maumivu ya Jua la Utosi na kuendelea na mashindano hayo
 Mshiriki Wa TMT, Moses Obunde (Mwenye Suti) akimpongeza Mshiriki Mwenzie Mzee Kapalata Mtawa kwa kuweza kuondolewa Kwenye Jua la Utosi na Kupelekwa Kivulini katika Shindano la TMT linaloendelea.
 Washiriki walioingia kwenye Jua la Utosi wakiwa mbele ya Meza ya Pilato huku mshiriki mmoja kutoka kwa washiriki hao aliyaaga mashindano ya TMT.
 Simanzi Zikianzia hapo sasa mara baada ya Washiriki kupunguzwa ili apatikane mmoja wa kuondoka
 Wakabaki wawili na hatimaye mmoja kati ya hao aliweza kuondolewa katika mashindano hayo
 Hatimaye Mshiriki Isalito Isaya Akaweza kurudi ndani ya Mjengo wa TMT kutokana na Kura zake kumzidi Mshiriki mwenzie Pendo ambaye aliweza kuaga mashindano hayo kutokana na kura kuwa chache
Baadhi ya Washiriki wa TMT wakimuaga Mshiriki mwenzao Pendo Edward (Katikati) ambaye aliweza kutolewa kwenye mashindano kutokana na kura kuwa chache.Picha Zote na Josephat Lukaza
--
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
Hatua ya mchujo katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limeingia wiki ya tatu ya mchujo sasa mara baada ya mshiriki mmoja kuaga shindano hilo wiki hii. Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limekuwa shindano bora ambalo kadri siku zinavyozidi kwenda linazidi kuteka nyoyo za watanzania wengi waliopo ndani na nje ya Nchi kutokana na utofauti wake na uzuri wake pia.
Mshiriki mmoja ambaye ni Pendo Edward aliweza  kuchomwa na jua la utosi lililompelekea kutoka kwenye shindano hilo kubwa la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo mpaka sasa washiriki kumi na tano (15) ndio wamebaki katika nyumba ya TMT na hali ya simanzi bado inaendelea katika nyumba ya TMT kwa wiki hii ambapo mshiriki mwingine atatakiwa kutoka.
Shindao la TMT limekuwa likivuta hisia za watanzania wengi waliopo ndani na Nje ya Tanzania kutokana na Utofauti wake na ubora wake na kupelekea watanzania wengi sana kufuatilia shindano hilo kwa ukaribu na umakini zaidi.
Hatimaye wiki hii Tanzania Movie Talents iliamua kuzindua Zoezi la kuwapigia kura washiriki wake kupitia ukurasa wetu wa facebook ambapo sasa watanzania na wapenzi wa TMT ambao wanauwezo wa kupata na kutumia internet sasa wanaweza kuwapigia kura washiriki waliowavutia kupitia ukurasa wetu wa facebook na vilevile kuendelea kuwapigia kura washiriki kwa kutumia simu zao za mkononi.
Jinsi ya Kumpigia kura Mshiriki umpendae kwa Kutumia Simu ya Mkononi Andika Neno "TMT" ikifuatiwa na namba ya ushiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano TMT 00 tuma kwenda 15678
Na Jinsi ya Kumpigia kura mshiriki kupitia ukurasa wetu wa facebook BOFYA HAPA  kwa kupata maelezo.



Comments