Msafara wa watu 25 wa                kikosi cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya                miaka 17 (Serengeti Boys) unaondoka kesho (Julai 28 mwaka                huu) kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mechi dhidi ya                Afrika Kusini (Amajimbos).
        Mechi hiyo ya marudiano                ya raundi ya pili itachezwa Jumamosi, Agosti 2 mwaka huu                kwenye Uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto, Johannesburg                kuanzia saa 9 kamili mchana kwa saa za Afrika Kusini.
        Timu hizo zilitoka                suluhu katika mechi ya kwanza iliyofanyika Julai 18 mwaka                huu kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es                Salaam. Mshindi atacheza raundi ya mwisho ya michuano hiyo                ya Afrika na mshindi wa mechi kati ya Misri na Congo                Brazzaville.
        Fainali za Afrika kwa                vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitafanyika mwakani                nchini Niger.
        Wachezaji wanaounda                kikosi cha Serengeti Boys katika msafara huo utakaoondoka                saa 2 usiku kwa ndege ya Fastjet ni Abdallah Jumanne                Shimba, Abdulrasul Tahil Bitebo, Abutwalibu Hamidu Msheri,                Adolf Mtsigwa Bitegeko, Ally Aziz Mnasi, Ally Shaban                Mabuyu na Athanas Enemias Mdamu.
        Wengine ni Badru Haji                Othman, Baraka Yusuph Baraka, Issa Backy Athuman, Juma                Ally Yusuph, Kelvin Longnus Faru, Martin Kiggi Luseke,                Metacha Boniface Mnata, Mohamed Mussa Abdallah, Omary Ame                Omary, Omary Natalis Wayne, Prospal Alloyce Mushin na Seif                Said Seif.
        Benchi la Ufundi                linaongozwa na Kocha Mkuu Hababuu Ally Omary akisaidiwa na                Stewart John Hall (Mshauri wa Ufundi), Peter Manyika                (Kocha wa makipa), Richard Yomba (Daktari), na Edward                Venance (Mtunza vifaa).
        Msafara wa timu hiyo                itakayorejea nyumbani Agosti 4 mwaka huu unaongozwa na                mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa                Miguu Tanzania (TFF), Khalid Mohamed Abdallah.
        BONIFACE WAMBURA
        OFISA HABARI NA                MAWASILIANO
        SHIRIKISHO LA MPIRA WA                MIGUU TANZANIA (TFF)
        
Comments
Post a Comment