Romelu Lukaku ameamua kufanya mazoezi na timu yake ya zamani kabla ya kuanza msimu mpya.MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Romelu Lukaku anajifua na klabu yake ya zamani ya Anderlecht kwa lengo la kujiweka fiti kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England.
Lukaku bado hajaungana na wachezaji wenzake kutokana na likizo aliyoipata baada ya kutoka katika fainali za kombe la dunia na timu yake ya Taifa ya Ubelgiji.
Mkali wa mabao: Mshambuliaji wa Ubelgiji, Lukaku alikuwa katika kiwango cha juu na klabu yake ya Everton alipokuwa anacheza kwa mkopo msimu uliopita.
Comments
Post a Comment