REAL MADRID YAFANYA KUFURU …PESA ZA USAJILI WA RODRIGUEZ, BALE NA RONALDO ZINAVUKA PESA ZILIZOTUMIWA NA AJAX KWA MUDA WA MIAKA 114
MSHAMBULIAJI wa Colombia na Monaco James Rodriguez ametanganzwa rasmi kama mchezaji wa Real Madrid na kuunda safu ghali zaidi ya ushambuliaji duniani.
Mchezaji huyo amesajiliwa kwa pauni milionoi 60. Ukichanganya na pauni milioni 86 ya Gareth Bale, pauni milioni 80 ya Ronaldo unapata hesabu ambayo haijawahi kufikiwa na timu kama Ajax ya Holland ambayo ndani ya miaka 114 imetumia pauni milioni183 katika manunuzi ya wachezaji kwa kipindi chote cha historia ya timu hiyo.
Kiasi hicho kilichotumiwa na Ajax kwenye usajili wao wa ndani ya miaka 114 ni pungufu kwa pauni milioni 43 ya mshiko uliotumiwa na Real Madrid kuwasajili washambuliaji hao watatu tu.
Usajili wa bei mbaya uliowahi kufanywa na Ajax ni Miralem Sulejmani (£13m), Marcelo (£5m, akiwa na umri wa 19), Raphael Varane (£8m, akiwa na umri wa 18), Daniel Carvajal (£4m, miaka 21) na Diego Lopes (£3m).
James Rodriguez aliyetwaa taji la mfungaji mabao mengi katika kombe la dunia huko Brazil amesaini wa miaka 6 na mabingwa hao wa Ulaya.
Rodriguez aligonga vichwa vya habari baada ya kufunga mabao 6 licha ya timu yake ya Colombia kubanduliwa nje ya kombe la dunia katika hatua ya robo fainali.
Comments
Post a Comment