Kipa                      mpya: David Ospina aliisaidia Colombia kufika Robo                      Fainali katika Kombe la Dunia kabla ya kutolewa na                      Brazil.
              KLABU ya Arsenal imekamilisha                          usajili wa kipa wa Nice, David Ospina kwa dau la                          Pauni Milioni 3.2, kwa mujibu wa kocha wa klabu                          hiyo ya Ufaransa, Claude Puel.                                                                                                                                        
                                            Ospina aliivutia The                                    Gunners kufuatia kuranya vizuri                                    akiidakia Colombia katika Kombe la                                    Dunia hadi kuifikisha Robo Fainali,                                    ambako walitolewa na wenyeji, Brazil.
                              Mlinda mango huyo mwenye umri wa                          miaka 25 anajiunga na timu hiyo ya Kaskaizni mwa                          London kwa mkataba wa miaka minne. Puel                          amezungumzia habari za kuondoka kwa Ospina                          alipohojiwa na Sky Sports na                          kusema: "Imethibitishwa, ndiyo. Akiwa na umri wa                          miaka 25 ni muhimu kwake kupata uzoefu wa                          mashindano mengine, hivyo ni uhamisho mzuri                          wake,".
                    Uwezo utamuweka mtu langoni:                David Ospina (kushoto) atatombea mamba na kipa wa sasa wa                kwanza wa Arsenal, Wojciech Szczesny
        Inafahamika kwa sasa kipa huyo                anakwenda kuchukua nafasi ya Lukasz Fabianski, ambaye                amejiunga na Swansea, kwenda kuwa wa pili nyuma ya kipa                namba moja wa sasa wa klabu hiyo, Wojciech Szczesny.
        Pamoja na hayo, kocha Arsene                Wenger amesema uwezo ndio utakaomfanya mmoja wao awe                kipa mamba moja wa klabu, huku Ospina akionekana kabisa                kuitaka kuwa chaguo la kwanza.
        "Unajua mwanzoni Szczensy                atakuwa mamba moja, kisha tena uwezo wa mtu ndiyo utaamua,                ikiwa Ospina ataonyesha ni bora, atacheza,"aliiambia ESPN
        
Comments
Post a Comment