
Liverpool                wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Ubelgiji Divock                Origi kutoka Lille kwa pauni milioni 10. Origi, 19,                amesaini mkataba wa miaka mitano, lakini atasalia Ufaransa                na klabu yake ya Lille kwa mkopo kwa msimu ujao na atakwenda                Anfield msimu wa 2015. Origi alicheza mechi zote za 
        Ubelgiji            katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 na alifunga bao pekee            katika mchezo dhidi ya Urusi. Alianza kucheza soka katika            klabu ya Genk kabla ya kuhamia Lille akiwa na miaka 15. Origi            anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Liverpool, baada ya            kumchukua Rickie Lambert, Adam Lallana na Dejan Lovren kutoka            Southampton, pamoja na Emre Can kutoka Bayer Leverkusen na            Lazar Markovic kutoka Benfica. 
Comments
Post a Comment