BENDI mbili kongwe kulizo zote zile za dansi, Msondo Ngoma Music Band "Baba ya muziki" na Mlimani Park Orchestra "Sikinde ngoma ya ukae" siku ya Idd Mosi zilionyeshana kazi kwenye viwanja vya TCC Club Chang'ombe.
Lilikuwa ni onyesho la Nani Zaidi ambapo mashabiki ndio waliochiwa waamue wenyewe ipi ni bendi bora zaidi. Hata hivyo, kwa jicho la kawaida ngoma ilikuwa droo.
Lilikuwa ni onyesho zuri la kiutu uzima lililosheheni ufundi wa hali ya juu huku ushabiki mithili ya ule wa Simba na Yanga ukitawala.
Pata picha za onyesho hilo.
Hassan Rehan Bitchuka akiongoza jahazi la Sikinde
Shaaban Dede wa Msondo akiimba kwa hisia kali
Hassan Moshi "TX Junior" moja ya nguzo za Msondo
Abdallah Hemba wa Sikinde akishambulia jukwaa
Jamwaka wa Sikinde katika Tumba
Joseph Bernad wa Sikinde akipuliza Saxphone
Waimbaji wa Msondo: Edo Sanga, Shaaban Dede na Juma Katundu
Juma Katundu (kushoto) na Hassan Moshi (kulia) wakishambulia jukwaa na mashabiki wa Msondo
Maswahiba! Kichuna wa Kimakua akiwa na Abdulfareed Hussein katika onyesho la Msondo na Sikinde
Hawa Msondo hawamalizi tu!!? ni kama anahoji mwimbaji wa Sikinde Hassan Kunyata
Mashabiki wakiselebuka
Masoud Masoud MC wa mpambano wa Msondo na Sikinde
Mpiga solo wa Sikinde Adolph Mbinga
Kazi inaendelea kwa mashabiki wa Msondo na Sikinde
Wanachama wa kundi la Bongo Dansi (BD) wakifuatilia mpambano
Meza ya wadau wa Bongo Dansi
Mwimbaji wa Sikinde Munsemba wa Minyigu
Hadi wazungu hawakubaki nyuma
Mikakati: Ridhwan Pangamawe wa Msondo akipeana mbinu na Shaaban Dede
Abdul Ridhwan "Panga mawe" wa Msondo akipiga solo gitaa kwa hisia kali
Roman Mng'ande "Romario" wa Msondo akifanya yake jukwaani
Shaaban Lendi wa Msondo akipuliza sax
Shukuru Majaaliwa akiimba kwenye jukwaa la Msondo
Waimbaji wa Sikinde
Mwimbaji mpya wa Msondo Twaha Mohamed
Mashabiki waliojazana mbele ya jukwaa la Sikinde
Sikinde wakishambulia jukwaa
Comments
Post a Comment