PICHA 20 ZA FUTARI YA ISHA MASHAUZI JUMAMOSI USIKU …palikuwa hapatoshi …mastaa kibao wahudhuria



PICHA 20 ZA FTARI YA ISHA MASHAUZI JUMAMOSI USIKU …palikuwa hapatoshi …mastaa kibao wahudhuria
PICHA 20 ZA FTARI YA ISHA MASHAUZI JUMAMOSI USIKU            …palikuwa hapatoshi …mastaa kibao wahudhuria

JUMAMOSI jioni, mkurugenzi wa kundi la Mashauzi Classic Modern Taarab, Isha Mashauzi, alifutarisha nyumbani kwake Hananasif, Kinonondoni jijini Dar es Salaam na kudhuriwa na watu kibao wakiwemo wasanii wa fani mbali mbali.

Ilikuwa ni tukio moja maridadi sana ambapo watu walipata nafasi ya kufanya dua, kabla ya kupata ftari na baadae kuwa na wasaa wa kuongea mawili matatu.

Kwa kuzingatia kuwa Mashauzi Classic hawatakuwepo jijini Dar es Salaam katika msimu wote wa sikukuu ya Eid el Fitr, ftari ile ikawa ni wasaa mzuri wa kutakiana kheri za sikukuu ambayo inatarajiwa kuanza Jumatatu au Jumanne kutegemea na mwandamo wa mwezi.

Pata picha kibao za tukio hilo

 Watoto wa Madrasa wakipata ftari
Hapa ilikuwa ni wasaa wa kupata dua
Dua inaendelea
Masupastaa wa movie za kibongo Gabo (kushoto) na Yussuf Mlela
Gabo akikaribishwa na meneja wa Mashauzi Classic, Ismail "Suma Raga" (kulia)
Kutoka kushoto: Gabo, Suma Raga, Kassim Mganga, Hashim Said
Mtoto wa Isha Mashauzi Ibtidaiyaht 
Mpiga kinanda wa Mashauzi Kalikiti Moto (kushoto) akiwa na fundi mitambo wao
 Msanii wa bongo fleva Kassim Mganga (kushoto) akihojiwa na TBC
Asha Manga (kushoto) na msanii wa bongo fleva Shetta wakipata ftari ya upendeleo baada ya kuchelewa kufika
Watu wa kila namna walihudhuria
Mwigizaji Hemed PHD akipata ftari
 Mtangazaji wa East Africa Radio Mwanne Othman akisaidaia kukarangiza mapocho pocho
Baadhi ya waalikwa
Waimbaji wa zamani wa Jahazi Modern Taarab Isha Mashauzi (kushoto) na Mwanne Othman
 Sehemu ya umati uliofurika nyumbani kwa Isha Mashauzi
Hemed na Isha katika picha ya pamoja baada ya ftari
Mama mzazi wa Isha Mashauzi Bi Rukia Juma
 Saluti5 ikipata wasaa wa kufanya mahojiano na TBC
 Shetta na mwimbaji wa Mashauzi Classic Hashim Said
Watu walikuwa ni wengi sana kiasi kwamba nyumba ilionekana ndogo

 



Comments