PICHA 11 ZA MASHAUZI CLASSIC ILIVYOPIGA SHOW YA KIHISTORIA MWANZA …Isha akamua nyimbo sita jukwaani, nyomi si la kitoto




PICHA 11 ZA MASHAUZI CLASSIC ILIVYOPIGA SHOW YA KIHISTORIA MWANZA …Isha akamua nyimbo sita jukwaani, nyomi si la kitoto
PICHA 11 ZA MASHAUZI CLASSIC ILIVYOPIGA SHOW YA            KIHISTORIA MWANZA …Isha akamua nyimbo sita jukwaani, nyomi si            la kitoto

MASHAUZI Classic Modern Taarab chini ya Isha Mashauzi, wameacha heshima ya aina yake jijini Mwanza kufuatia onyesho lao la Idd Mosi lililofurika mashabiki wa muziki kupitiliza.

Onyesho hilo lililofanyika kwenye jengo la Buzuruga Plaza, liliwapeleka mashabiki msobe msobe mwanzo hadi mwisho huku waimbaji Hashim Said, Abdulmalick Shaaban, Zubeida Mlamali, Asia Mzinga na Thania Msomali wakitesa kwa nyakati tofauti.

Isha Mashauzi kwa mara nyingine tena (si ya kwanza, ya pili wala ya tatu) akadhihirisha kuwa ana pumzi za kipekee za kusimama jukwaani na kuimba nyimbo nyingi mfululizo huku pia akilisakata sebene step kwa step. Haishangazi kwanini alikuwa mburudishaji bora wa kike wa mwaka  kupitia Kilimanjaro Tanzania Music Awards.

Mwimbaji huyo ambaye pia anashilikilia tuzo ya mwimbaji bora wa kike, alikamua jumla ya nyimbo zake sita, lakini pia alitupia vipande vya nyimbo mbali mbali za bongo fleva kila baada ya wimbo mmoja, hali iliyozidi kuwapagawisha mashabiki wa Mwanza.

Isha aliipanda jukwaani saa 5.30 za usiku akaimba nyimbo tano mfululizo "Nani Kama Mama", "Mamaa Mashauzi", "Mapenzi hayana Dhamana", "Viwavi Jeshi" na "Sura Surambi".

Hakuishia hapo, Isha alipumzika kwa dakika chache tu  akimpisha Asia Mzinga na wimbo mpya "Wema Hauozi" kabla ya kurejea tena jukwaani kuimba wimbo "Asiyekujua Hakuthamini".

Hakika lilikuwa ni onyesho la kutakata na wala haikujalisha kuwa ndani ya jiji la Mwanza kulikuwa na onyesho lingine kubwa kutoka kwa bendi ya Extra Bongo iliyofanya vitu vyake kwenye ukumbi wa Jembe ni Jembe.

 Mwimbaji Abdumalick Shaaban
Mwimbaji Asia Mzinga
 Isha Mashauzi akiimba mbele ya umati mkubwa wa mashabiki
 Isha Mashauzi akiendelea kufanya makamuzi
 Huyu ni mpiga bass anayejulikana kama J Four "John Cena"
Kalikiti Moto katika kinanda
Mpiga solo Hassan Kubea
Sehemu ya umati mkubwa uliofurika ukumbi wa Buzuruga
Waimbaji Thania Msomali (kushoto) na Zubeida Malick
Meneja wa Mashauzi Classic Ismail "Suma Raga" akifuatilia onyesho kwa makini

 



Comments