PICHA 10 ZA SHOW YA TWANGA PEPETA MANGO GARDEN …wasanii wapya watambulishwa, Diouf atoweka, Asha Baraka atoa kauli
ONYESHO la Twanga Pepeta siku ya Idd Mosi pale Mango Garden, lilikuwa moja ya maonyesho bab kubwa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Twanga Pepeta walipiga show ya nguvu, wakatambulisha madansa wanne wapya kutoka Extra Bongo: Sabrina, Maria, Danger Boy na Hamza Mapande.
Hata hivyo watu wengi waliofika kwenye onyesho hilo, hawakufanikiwa kumuona rapa Msafiri Diouf kama ilivyokuwa imeelezwa hapo awali kuwa msanii huyo naye anarudishwa kundini na atatambulishwa siku ya Idd Mosi.
Hakukuwa na sababu zozote zilizotolewa ukumbini hapo juu ya kukosekana kwa Msafiri Diouf na hivyo kuwafanya washabiki wengi wabaki njia panda.
Hata hivyo, baadae Saluti5 iliongea na mkurugenzi wa Aset Asha Baraka ambaye alikuwa na haya ya kusema kuhusu rapa huyo:
"Diouf ameomba atambulishwe rasmi Jumamosi Mango Garden kwa vile anataka ashuke na vitu vipya.
"Ameshiriki mazoezi kwa siku 2, tulitarajia tumtambulishe siku ya Idd Mosi lakini tumeamua kumfanyia tukio maalum Jumamosi ijayo ili ajinoe zaidi." Alimaliza Asha Baraka.
Comments
Post a Comment