Arsene Wenger akipozi katika picha na nyota   wa  New York Red Bulls, Thierry Henry (wa pili kushoto).
  KOCHA wa Asernal, Mfaransa,  Arsene Wenger   ameweka wazi kuwa wachezaji wake watatu walioshinda kombe la dunia wana   uwezekano mkubwa wa kukosa mechi ya ufunguzi ya ligi kuu soka nchini England   dhidi ya Crystal Palace.
  Mesut Ozil, Per Mertesacker na Lukas Podolski   wapo likizo mpaka Agosti 11 mwaka huu baada ya kuisaidia Ujerumani kutwaa kombe   la dunia nchini Brazil.
  Wachezaji wa Asernal wakifanya mazoezi kwenye   uwanja wa  New York Red Bulls kuelekea mechi ya kirafiki kesho jumamosi.   
Arsene Wenger akizungumza na shujaa wa zamani wa   washika bunduki Thierry Henry ambaye kwasasa anaichezea New York Red   Bulls
Wenger wachezaji wake watatu washindi wa kombe   la dunia wanaelekea kukosa mechi ya kwanza ya msimu.
  Mfaransa huyo alisema: "Nimewapa likizo nzuri   kwasababu nina uzoefu na wachezaji waliokuwa katika fainali ya kombe la dunia.   Unahitaji kupumzika".
  "Watakuwa tayari?  Mertesacker anajiandaa   vizuri - lakini kwa mchezo wa kwanza Agosti 16 sidhani kama watakuwa   tayari".
  Wenger aliyekataa kuthibitisha kama amemuadhibu   Jack Wilshere baada ya kupigwa picha akivuta sigara, pia aliwaibukia FIFA na   kuwaambia wanatakiwa kufirikia upya ratiba yao kwasababu imempa ugumu katika   kikosi chake.
    Abou Diaby akijiweka fiti kwenye mazoezi mjini   New York.
Comments
Post a Comment