Tumelianzisha                tena! Raheem Sterling anajua wazi kuwa anatakiwa                kujithibitsha mwenyewe kuwa ni bora.
          LICHA                ya kuwa miongoni mwa wachezaji wachache wa England                waliorudi na heshima kutoka kombe la dunia, Raheem                Sterling amesisitiza kuwa anahitaji kuonesha kiwango                kikubwa katika klabu yake ya Liverpool msimu ujao.
          Nyota                huyo kinda mwenye miaka 19 alikuwa miongoni mwa wachezaji                wa Liverpool waliokaribia kutwaa ubingwa wa ligi kuu                ambapo walimaliza pointi mbili nyuma ya mabingwa                Manchester City.
          Sterling                amejiunga na kambi ya mazoezi iliyopo Boston akijua wazi                kuwa kusajiliwa kwa wachezaji wapya kunamaanisha nafasi                yake haina uhakika.
          Akizungumza                na LFCTour.com, alisema: "Bado natakiwa kujithitisha                mwenyewe, kocha ameleta wachezaji ambao wenye uwezo wa                kucheza nafasi kama yangu, natakiwa kumuonesha kocha na                kujituma zaidi ili kupata namba ya kudumu katika timu".
        Kivutio:                Raheem Sterling amekuwa na mvuto tangu alipowasili katika                kambi ya Liverpool iliyopo Boston.
          "Hii                ni klabu ya juu ikiwa na wachezaji wa kiwango cha juu,                ambao wamekuja kushindana siku zote. Hakuna utofauti sana                kwenye mazoezi"
          "Kuna                vitu vingi kutoka kwangu. Nahitaji kujituma na natumaini                nitapata namba msimu ujao na kufanya kila linalowezekana                kuisaidia klabu".
          Sterling                alijitambulisha mwenyewe katika ulimwengu wa soka baada ya                kuonesha kiwango cha huu kwenye mechi ya ufunguzi ya kombe                la dunia dhidi Italia ambapo walilala mabao 2-1, lakini                kijana huyo mwenye kipaji alicheza mpira mwingi mno.
        Ushindani:                Wachezaji wapya waliosajiliwa ni pamoja na Lazar Markovic                (kushoto) ambao watampta presha Sterling
        Raheem                Sterling akichuana na mchezaji mwenzake wa England  Daniel                Sturridge wakati wa mazoezi  Boston.
        
Comments
Post a Comment