‘NDEGE’ WA MANCHESTER UNITED WAZIDI KUPEPERUKA … Stefan de Vrij ajiandaa kwenda Lazio



'NDEGE' WA MANCHESTER UNITED WAZIDI KUPEPERUKA … Stefan de Vrij ajiandaa kwenda Lazio
'NDEGE' WA MANCHESTER UNITED WAZIDI KUPEPERUKA … Stefan            de Vrij ajiandaa kwenda Lazio

BEKI wa kimataifa wa Holland Stefan de Vrij ambaye ilionekana kama yuko njiani kwenda Manchester United, sasa anatarajiwa kujiunga na Lazio ya Italia.

Nyota huyo anayeichezea Feyenoord, alicheza kila mchezo wa kombe la dunia chini ya kocha Louis van Gaal na iliaminika kuwa ataenda kuungana na kocha huyo Old Trafford.

Hata hivyo Feyenoord imethibitisha Jumatatu hii kuwa De Vrij atajiunga na Lazio kwa dau la pauni milioni 6.7.

De Vrij mwenye umri wa miaka 22 ameichezea Holland mara 19 akiwa kama beki wa kati lakini pia ana uwezo wa kucheza kama beki wa kulia.

United inaendelea na harakati zake za kumnasa beki wa Arsenal Thomas Vermaelen kama moja ya malengo ya kuziba nafasi za Nemanja Vidic na Rio Ferdinand.



Comments