Kocha wa Mwadui fc, Jamhuri Kiwhelo 'Julio'
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TIMU ya Mwadui fc ya Shinyanga inatarajia kuanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi daraja la kwanza unaotarajia kuanza mwezi Octoba mwaka huu.Kocha mkuu wa klabu hiyo, Jamhuri Musa Kiwhelu 'Julio' amesema mazoezi hayo yataanza katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa Mwadui watahudhuria.
"Tunaanza mazoezi kesho katika viwanja vya Leaders kwa baadhi ya wachezaji wa Mwadui kuhudhuria.Tunatarajia kuwa na timu bora yenye ushindani mkubwa, kwahiyo Kesho saa kumi jioni tunaanza mazoezi," Alisema Julio.
Julio aliongeza kuwa klabu yake inahitaji kufanya usajili wa wachezaji wengine kwasababu muda unakimbia sana.
Kocha huyo alibainisha kuwa wameamua kuitisha majaribio ya wachezaji, hivyo kwa wote wanaojiona wana vipaji wafike kesho Leaders.
"Wachezaji walioachwa Simba, Yanga wafike kujaribiwa. Tunawakaribisha watu wote wenye uwezo," Alisema Julio.
Comments
Post a Comment