
NA FULLSHANGWE
        KATIKA historia yake, klabu              ya Simba haijawahi kuwa na uwanja wake wa mazoezi, hivyo              kujikuta anahangaika miaka nenda rudi.Lakini kwasasa unaweza              kusema imedhamiria kujenga uwanja wa mazoezi maeneo ya Bunju              jijini Dar es salaam.Ismail Aden Rage alipokaribia kumaliza              muda wake alianza mchakato wa kujenga uwanja wa Bunju              akisema wanataka kupata sehemu ya kufanyia mazoezi.Pia              alisema wanakusudia kujenga hosteli za kuishi wachezaji              ikiwa ni mkakati wa kupunguza gharama ya kuweka wachezaji              hotelini.
        Uongozi mpya chini ya Rais              Evans Elieza Aveva alisema uko tayari kuendeleza ujenzi huo              ulioanzishwa na Rage.
        Mpaka sasa nyasi              zilishapandwa na muonekano wa uwanja uko kama unavyoonekana              pichani juu.
        
Comments
Post a Comment