MPAMBANO WA MSONDO NA SIKINDE IDD MOSI NI SHIDA …bendi zahofia juju, zasisitiza kila bendi na jukwaa lake
KWA mara nyingine tena, bendi pinzani za Mlimani Park "Sikinde Ngoma ya Ukae" na Msondo Ngoma Music Band "Baba ya Muziki" zimekataa wazo la kutumia jukwaa moja kwenye mpambano wao siku ya Idd Mosi TCC Club Chang'ombe.
Mara ya mwisho bendi zilipopambana kwenye uwanja huo huo wa TCC Club katika sikukuu ya X-Mas, kila bendi ilitumia jukwaa lake na seti yake ya vyombo.
Safari hii kulikuwa na wazo lililotaka bendi hizo kutumia jukwaa moja ili kuonyesha mshikamano, lakini viongozi wa Msondo na Sikinde walipinga vikali wazo hilo na kusisitiza kuwa kila bendi na jukwaa lake, kila bendi na vyombo vyake.
Mratibu wa onyesho hilo Joseph Kapinga ameiambia Saluti5 kuwa bendi hizo zinaogopa kutumia jukwaa moja kwa kuhofia hujuma za kuharibiana 'setting' za vyombo pamoja na kupigana juju.
Kapinga amesema viongozi bendi hizo wamedai linapokuja suala la mpambano wa Msondo na Sikinde hakuna hakuna kitu kinaitwa "kuaminiana".
Pichani juu ni namna mashabiki walivyofurika kwa wingi kwenye mpambano wao uliofanyika X-Mas ya mwaka jana.
Pambano la Msondo na Sikinde limedhaminiwa na Konyagi na www.Saluti5.com
Comments
Post a Comment