KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amethibitisha kuwa mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo, Didier Drogba anarudi darajani.
Nyota huyo raia Ivory Coast aliitumikia Chelsea kwa miaka 8 na kuondoka mwaka 2012 ambapo alijiunga Galatasaray ya Uturuki baada ya kutwaa kombe la UEFA dhidi ya Bayern Munich.
Ingawa ana miaka 36 kwasasa, Mourinho anaamini bado anaweza wa kucheza ligi kuu nchini England na michuano ya kimataifa.
"Tunalifikiria hilo," Mreno huyo aliwaambia waandishi wa habari baada ya kuulizwa uwezekano wa Drogba kurudi.
"Tunahitaji kushinda mechi na kushinda makombe na Didier ni moja ya washambuliaji bora barani Ulaya,".
"Bado anao uwezo wa kucheza ligi kuu na tunalifikiria sana hilo na hatuendeshwi kwa hisia".
"Kama unamrudisha, si kwasababu yeye ni Didier au alifunga magoli mengi muhimu katika historia yake Chelsea, au kwasababu nahitaji msaidizi, hapana, namrudisha na maamuzi yamekuja mapema kwasbaabu yeye kama mchezaji anaweza kuifanya timu kuwa imara".
Comments
Post a Comment